Athari ya Jinsiaya Mtunzi katika Usawiri wa Wahusika katikaRiwaya zaKiswahili:Mifano kutokana na Riwaya ya Nyuso za Mwanamke na Nguu za Jadi.

  • Dkt.Rose Kawira Chuo Kikuu cha Mount Kenya
  • Dkt.Aggrey Wanyama Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta
  • Mary Nyambura Mwangi Chuo Kikuu cha Mount Kenya
Keywords: Chanya, Hasi, Jinsia, Kweza, Tweza, Usawiri, Ubabedume, Wahusika

Abstract

Kila mwandishi huathiriwa na sababu mbalimbali katika usawiri wa wahusika kwenye utunzi wake. Ni kwa sababu hii basi tumeweza kuchunguza athari ya jinsia ya mwandishi katika usawiri wa wahusika katika riwaya za Kiswahili. Tumeweza   kubainisha jinsi usawiri wa wahusika katika riwaya huathiriwa na jinsia ya mwandishi. Hii ni kwa sababu kuwa wahusika katika riwaya huwa wengi na husawiriwa kwa njia mbalimbali. Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza athari ya jinsia ya mwandishi katika usawiri wa wahusika katika riwaya ya Kiswahili. Lengo hili lilitimizwa kupitia kwa lengo mahususi ambalo ni; kutathmini athari ya jinsia ya mwandishi katika usawiri wa wahusika kwa njia chanya au hasi ili kuwakweza au kuwatweza. Nadharia iliyotumika katika utafiti huu ni nadharia ya Ufeministi wa Kiafrka iliyoasisiwa na Steady (1981). Utafiti huu ulifanyika maktabani. Data ilikusanywa kupitia usampulishaji lengwa kutoka katika riwaya teule ambazo ni Nyuso za Mwanamke (2010) Said A Mohamed na Nguu za Jadi(2022) Clara Momanyi. Data hii imechanganuliwa kwa njia ya maelezo kwa mujibu wa malengo ya utafiti na mihimili ya nadharia teule. Utafiti huu utawafaidi wasomi, watafiti na wahakiki wa kazi za kifasihi kwa kuwa utachangia kujaza mapengo katika utafiti hasa kuhusu masuala ya kijinsia. Vilevile, tumekusudia utafiti huu uweze kuwafaidi wahakiki na wasomi katika kuzitafiti kazi nyinginezo za kifasihi. Mbali na hayo, utafiti wetu utatumika kama katika marejeleo kwa watafiti wa masuala ya kijinsia wa siku zijazo katika uendelezaji tafiti zao.

References

Chesaina, C. (1987). Women in African Drama.Tasnifu ya PhD.Chuo Kikuu Cha Leeds.
De Beavour, S. (1949). The Second Sex.London: Pan Books Publisher.
Engels, F. (1975). The Origin of the Family Private Property and the State.New York: Pathfinders Press Inc.
Figes, E. (1978). PatriarchalAttitudes.London: Virago Press.
Lugano, R.S. (1989). Mwanamke katika Riwaya ya Kezilahabi: Tasnifu ya M.A Chuo Kikuu cha Kenyatta. (Haijachapishwa)
Mavisi, R. (2007). Usawiri wa wahusika wa kike katika kazi za Z. Burhani.Tasnifu ya M.A. Chuo Kikuu cha Kenyatta. (Haijachapishwa)
Momanyi, C (2021). Nguu za Jadi.Nairobi: Queenex Publsihers Limited.
Millet, K. (1969). Sexual Politics.London: Virago press.
Said, A.M. (2010). Nyuso za Mwanamke.Nairobi. Longhorn publishers.
Steady, F.C. (1981). Black Women Cross Culturally.Cambridge: Mass Scherkman Publishing Co.Inc.
TUKI, (2013). Kamusi ya Kiswahili Sanifu.Nairobi: Oxford University Press.
Wamitila, K.W. (2002). Uhakiki wa Fasihi: Nairobi.Phoenix Publisher.
Published
2024-10-14