Ulinganifu na Ulinganuzi wa Kimtindo katika Ujenzi wa Upembezwaji wa Mwanamke katika Bunilizi Tuele za Clara Momanyi na Omar Babu
Abstract
Jamii nyingi za Kiafrika humpembeza mwanamke kwa kumweka katika ngazi za chini huku mwanamume akiwekwa kwenye ngazi za chuni.. Upembezwaji wa mwanamke katika tungo za kifasihi na katika maendeleo ya jamii ni matokeo ya mwingiliano wa fahamu tambuzi na fahamu bwete za mtunzi hasa kwa mujibu wa utamaduni wa jamii lengwa. Mwingiliano huu wa ufahamu tambuzi na ufahamu bwete unaekezwa kwa makusudi katika utunzi wa tungo mahususi kama ilivyo kwenye tungo za Momanyi ‘Ngome ya Nafsi’katika Mayai Waziri wa Maradhi na Hadithi Nyingine (2004), Tumaini (2006) na Nakuruto (2010) nazo za Babu ni Kala Tufaha (2007), Heri Subira (2010) na ‘Ndoa ya Samani’ (2011. Data ya usomi huu ilitokana na usomaji wa bunilizi hizi maktabani. Tuliweza vilevile kutumia mitandao kurutubisha utafiti wetu. Hatimaye, ilichambuliwa kuzingatia mihimili ya nadharia ya Ufeministi wa Kiafrika. Hivyo, ni kwa jinsi gani watunzi Momanyi na Babu wanarandana kimitindo katika ujenzi wa maudhui ya upembezwaji wa mwanamke kisanii katika jamii? Je, kuna naman ambavto wanatofautiana katika ususi wa kazi zao? Ni vipi ambavyo mwanamke anapembezwa kiutunzi katika kazi teule? Maswali haya ndiyo tulipania kuyajibu katika makala haya.
References
Babu, O. (2010). Heri Subira. Nairobi: Oxford Publishers.
Bank, O. (1990). Faces of Feminism. A study of Feminism as a Social Movement. Basil Blackwell: USA.
Chacha, W. C. (2013). ‘Taswira ya mwanamke katika tamthilia za Nguzo Mama na MamaEe’. Tasnifu ya Umahiri, Chuo Kikuu cha Nairobi. (Haijachapioshwa.)
Chesaina, C. (1987). ‘Women in African Drama: Representation and Role’. Tasnifu ya Uzamifu, University of Leeds. (Haijachapishwa).
Kamwara, K., (2022). ‘Ujenzi wa Ujitambuzinafsia wa Jinsia na Upembezwaji wa Mwanamke katika Bunilizi za Clara Momanyi na Omar Babu. Tasnifu ya Uzamifu Chuo Kikuu cha Nairobi,. (Haijachapishwa
Kamwara, K., (2016). ‘Mtazamo Mpya katika Sauti ya Kike katika Riwaya ya Kiswahili’. Tasnifu ya Uzamili Chuo Kikuu cha Mount Kenya. (Haijachapishwa).
Mboya, L. A., Mohochi, E. S., & Kisurulia, S. (2018). ‘Dhuluma kama Kichocheo cha Mzinduko wa Wanawake katika Riwaya ya Kiswahili’. Rongo: Rongo University Press. (http://respository.rongovasity.ac.ke/handle/123456789/1860).
Mikell, G., (1997). African Feminism: The Politics of Survival in Sub-Sahara Africa.
Mji?: University of Pennsylvania Press.
Mohochi S., et. (2018). ‘Dhuluma kama Kichocheo cha Mzinduko wa Mwanamke katika Riwaya ya Kiswahili’. Makala ya Chuo Kikuu Cha Rongo.
Momanyi, C. (2006). Tumaini. Nairobi: Vide-Muwa publishers.
Momanyi, C. (2009). Nakuruto. Nairobi: Longhorn publishers.
Musyoka F. M. (2011). ‘An Analysis of the Woman in Gender Role-Play Dynamics in Kenyan Kiswahili Drama.’ Tasnifu ya Umahiri. Chuo Kikuu cha Nairobi. (Haijachapishwa.)
Hamadi, M. (9.7.2019). ‘Mwanamke Bomba’ (Msururu wa Vipindi vya Televisheni vya ‘Citizen Kenya”). (https://youtu.be/FrBDtjx_SM).
Swaleh, A. (2011). ‘A Critique of the Mapping and Construction of Gender Identity and Authority in Selected Kiswahili Novels’.Tasnifu ya Umahiri. Chuo Kikuu cha Nairobi. \
Wafula,R.M.naK. wa Njogu(2007).NadhariazaUhakikiwaFasihi.Nairobi:Jomo KenyattaFoundation.
Wamitila, K. W. (2002). Uhakiki wa Fasihi; Nadharia na Mbinu.Nairobi: Phoenix Publishers.
Author(s) and co-author(s) jointly and severally represent and warrant that the Article is original with the author(s) and does not infringe any copyright or violate any other right of any third parties and that the Article has not been published elsewhere. Author(s) agree to the terms that the IJO Journal will have the full right to remove the published article on any misconduct found in the published article.