UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI:MFANO WA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI

  • JACKLINE NJERI MURIMI
  • Jude Muli Mukuta Chuo Kikuu cha Mount Kenya

Abstract

Masuala ibuka ni mambo yanayoangaziwa na kupewa kipau mbele katika jamii ya leo na aghalabu yalipuuzwa katika miaka ya zamani. Fasihi kama zao la wakati hubadilika jinsi jamii inavyobadilika ili iyamulike masuala mapya yanayoibuka katika jamii husika. Masuala haya ni pamoja na usawa katika jamii, haki za binadamu na mengine mengi. Utafiti huu umelenga kuonyesha jinsi haki za watoto zinavyokiukwa katika fasihi kupitia riwaya mbili teule ambazo ni:Chozi la Heri (2017) ya Assumpta K.Matei na Nguu za jadi (2021) ya Clara Momanyi. Ili kukamilisha lengo hili kuu, malengo mahususi matatu yalizingatiwa.Malengo hayo ni pamoja na; Kujadili jinsi ukiukaji wa haki za watoto unavyojitokeza katika riwaya teule,kutathmini madhara yanayotokana na ukiukaji wa haki za watoto katika riwaya teule na kuchanganua njia mbadala zinazoweza kutumika ili kuondoa ukiukaji wa haki za watoto katika jamii. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya uhalisia ambapo mihimili ya nadharia hii ilitusaidia kufikia malengo ya utafiti huu.Utafiti huu ulichukua muundo wa kimaelezo. Data ilikusanywa kule maktabani pale ambapo riwaya teule zilisomwa pamoja na tasnifu mbalimbali ili kurutubisha utafiti. Data ilichanganuliwa kwa njia ya kimaelezo kwa kuzingatia malengo na maswali ya utafiti pamoja na nadharia ya uhalisia.Uteuzi wa kimakusudi ulitumika katika utafiti huu kuteua riwaya ya Chozi la Heri na Nguu za Jadi. Utafiti huu utasaidia katika kuibua mapendekezo ambayo yatasaidia watengenezaji sera wanaojihusisha na suala la ukiukaji wa haki dhidi ya watoto,vilevile,utafiti huu utakuwa na mchango mkubwa katika taaluma ya elimu kwani utaihamasisha jamii kuhusu dhima ya fasihi ikiwemo kuyamulika matatizo yanayotokea katika jamii na kuyatafutia suluhu. Zaidi ya hayo, utafiti huu utawanufaisha waandishi wa kazi za fasihi kwani utawasaidia katika kutambua masuala nyeti katika jamii na namna ya kuyatatua.

References

Amulenga, C.M. na Amulenga, A.V. (2009) Solving Problems Occuring in Early Marriages. Nairobi: Focus Publishers
Atieno, W. (2014) ‘Mama ajifungua ndani ya TukTuk’. Taifa Leo, Septemba 9, kur.1,2
Bakize, L.. (2014). Utangulizi wa Fasihi ya Watoto. Dar es Salaam: Maccony Printing Press.
Behnam, N. (2008) ‘Kikanda, jamii na watoto’:Ripoti ya Kikanda ya kuanza kujifunza:Kuwawezesha jamii kuhusu ustawi wa watoto.Washington,DC.
Boss, P. (1998) Family Stress Management. Newbury Park, California: Sage Publications.
Burke, C. (1999) Covenanted Happiness, Love and Commitment in Mariage, 2nd Ed. New Jersey: Screptree Publishers.
Bronfenbrenner,U.(1979).’Elimu ya ustawi na uhusiano wa binadamu na mazingira’.Asili na desturi ya kutathmini vijiji kushiriki.Cambridge,MA:Uandishi wa Chuo Kikuu cha Harvard.
Cancer Global Statistics (2014).www.int/media centre/factsheets/fs297/en/.
Chambers,R. (1994).’Asili na desturi ya kutathmini vijiji kushiriki’.Maendeleo Duniani, 22.953-969’.
Chapman, R. (1982) The Language of English Literature. London: Edward Arnold Publishers.
De Genors, M.K (2008) Inmate, Relationship, Marriage and Families. Seventh edition.New York:Mc Grace Hill.
Drabble, M. (1995) The Oxford Companion to English Literature.New York: Oxford University Press.
Farouk, M.T. (1974) Uchambuzi wa Maandishi ya Kiswahili. Nairobi: Oxford University press.
Gitau, E. (2014) ‘Unyanyasaji Dhidi ya Wanaume katika Fasihi Andishi ya Kiswahili’.Tasnifu ya uzamili Chuo kikuu Cha Kenyatta.
Habwe, J.H. (2005) Paradiso. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.
Johnson, T. (2002) “ Violence and Abuse of Women and Girls in Kenya, Population Communication Africa.Nairobi: New World Printers.
Karanja, D.W. (2008). Usawiri wa Masuala-Ibuka katika hadithi za watoto.Tasnifu ya uzamili. Chuo kikuu cha Kenyatta.
Khamis, S.A. (2012) “ Riwaya Mpya ya Kiswahili. Utandawazi au Utandawizi? Lugha ya Riwaya Mpya Ya Kiswahili Inavyodai”. Bayreuth University.
Krueger, A. Thompson, G. na Crispin, V. (2013).’Kufijunza kutoka kwa mifumo ramani ya kulinda watoto na uchambuzi katika Afrika Magharibi’: Maana ya Utafiti na Sera.Sera za Kimataifa,5,47-55.
McKay, S., na Mazurana, D. (2004).’Wako wapi wasichana?’ Montreal, Canada: Kituo cha Kimataifa kwa Haki za Binadamu na maendeleo ya Kidemokrasia.
Panter-Brick, C., na Leckman, J. (2013). Tangazo mfululizo la Mhariri: Kuimarisha kwa ustawi wa mtoto –Njia zilizounganika kwa hali njema.Jarida la Saikolojia na Taaluma,Tiba ya Ugonjwa wa Akili kwa Watoto, 54,333-336.
Thompstone, G. (2010). Mapping na Uchambuzi wa mfumo wa kulinda watoto nchini Sierra Leone.Hong Kong,China: Watoto wa mpakani (Child Frontiers).
UNPD. (2013) Dalili za Umaskini na Maendeleo, Sierra Leone.Imepatikana kutoka hdstats.undp.org
UNICEF. (2013). Ukeketaji na Kutahiri wanawake : Maelezo ya takwimu na ugunduzi wa mienendo ya mabadiliko.New York, NY: Mwandishi.
UNICEF,UNHCR,Kulinda Watoto (Save the Children), na Maono Duniani (Maono ya Dunia).(2013).Njia bora ya kuwalinda watoto wote: Nadharia na Mazoea ya mfumo ya kulinda watoto,ripoti ya mkutano.New Delhi, India: Mwandishi.
Wessells, M.G. (2006). Wanajeshi watoto: Kutoka kwa Vurugu hadi Kulindwa. Cambridge, MA: Uandishi wa Chuo Kikuu cha Harvard.
Wessells, M.G. (2009a). Je, tunajifunza nini kuhusu kulinda watoto katika jamii? Kikanda cha mapitio ya ushahidi juu ya jamii kuhusu utaratibu wa kulinda watoto katika mazingira ya kibinadamu na maendeleo.London, England: Kulinda Watoto (Save the Children).
Whitney,S.D., Tajima, E.A.,Herrenkohl,T.I.,& Huang, B. (2006). Defining child abuse: Exploring variations in ratings of discipline severity among child welfare practotioners. Child and Adolescent Social Work Journal, 23, 316-342.
Yeo.L.S., & Choi, P.M. (2011). Cognitive-behavioural therapy for children with behavioural difficulties in the Singapore mainstream school setting. School Psychology International,32,616-631.
Published
2024-05-17