ATHARI ZA UDHANAISHI WA KIDINI KWA VIJANA KATIKA RIWAYAZA PARADISO NA KIDAGAA KIMEMWOZEA

  • JACKLINE NJERI MURIMI
  • Solomon Muli Chuo Kikuu cha Mount Kenya

Abstract

Suala la imani katika Mungu ni nyeti na linatiliwa maanani na binadamu katika tamaduni mbalimbali kote duniani kama njia mojawapo  ya kujaribu kutafuta majibu ya changamoto anazokubana nazo kila uchao. Katika jamii nyingi za kiafrika,dini ni mfumo wa maisha (Mbithi 2011 )ambapo kila mwana jamii alihitajika kushiriki. Hata hivyo, suala hili la kidini linaonekana kuwatamausha vijana wengi na kufifisha imani yao katika dini.                                                                                                                                                                        Hivyo ,utafiti huu ulinuia kuchanganua  baadhi ya athari za udhanaishi  wa dini kwa vijana kwa kurejelea riwaya ya Paradiso na Kidagaa Kimemwozea  zilizoandikwa na  John Habwe na Ken Walibora mtawalia kwa kuchunguza jinsi John Habwe na Ken Walibora wanavyoangazia udhanaishi wa kidini katika jamii .

Katika kulizamia suala hili makala hii iliongozwa na nadharia ya udhanaishi iliyoasisiwa na Mwanathiolojia kutoka Denmaki(1813-1855),Fredrick Nietzsche,Martin Heidegger,Gabriel Marcel na Karl Jaspers waliotokea karne ya 20 na Jean Paul Satre Mfaransa aliyetokea baada ya vita vya pili vya dunia.  Mihimili yake ilisaidia kufikia malengo ya yetu. Mihimili mikuu ya nadharia ya udhanaishi ni pamoja na;kutilia mkazo matatizo halisi yanayomsibu mwanadamu na kuwa na imani ya kijozi juu ya imani ya kuishi, inapalilia kutokuwepo kwa mungu na uumbaji wake wa ulimwengu,inatilia mkazo kuwa juhudi za mtu kujisaka au kujaribu kupambana na maisha huishia katika mauti,  maudhui yake ni kama vile uhuru wa mtu binafsi kuweza kufikiri halafu kutoa jawabu lake. Nadharia husimulia taabu na kuchoka na hali ambazo husumbua yanayotatiza mwana wa adamu,  nadharia hii inajadili mkengeuko,nadharia hii inachora taswira ya mateso anayopitia mwanadamu duniani,  nadharia hii inatilia mkazo kuwa maisha yamejawa na utupu na kihoro hasa kuhusu siku za kesho.Maisha yamejawa na ubwege na huhakikisha binadamu kuwa mwisho wa maisha ni kifo.Nadharia hii ilifaa utafiti kwani ilitumika kueleza jinsi baadhi ya vijana waumini wavavyoyaona maisha jambo ambalo linawafanya watamaushwe na dini kila uchao. Nadharia hii ilitumika kupambanua ukweli wa je ni lipi ambalo baadhi ya vijana katika jamii wamejua hivi karibuni ambalo mababu zao hawakufahamu hapo awali?Utafiti ulifanyika maktabani kuliko na vitabu, majarida,matini na magazeti na wa mtandaoni ambapo data ilipatikana  kutokana na tasnifu zilizoandikwa kuhusu mkengeuko wa imani za kidini.Sampuli ya kimaksudi ilitumika  katika kuteua riwaya ya Paradisona Kidagaa Kimemwozea. Mbinu anuwai za kimaelezo zilitumika katika kuchambua data na kuiwasilisha kwa lugha ya nadhari kuambatana na lengo la utafiti. Maarifa yaliyopatikana katika utafiti huu yatakuwa na mchango mkubwa katika maarifa yaliyopo kuhusu vijana na  masuala ya dini katika jamii.

References

Camus, A(1984). The Rebel: Hamish Hamilton, Loudon.
------------(1961)Resistance, RebellionandDeath.Translated by Justin O’Brien. New York:Knopf
Habwe, J. (2000). MaishaKitendawili.Nairobi.Jomo Kenyatta Foundation
-------- (.2005).Paradiso.Nairobi; The Jomo Kenyatta Foundation.
International Bible Society (1973). HolyBible:New International Version.New York.
Katiba ya Kenya (2010).GovermentPrinters.Nairobi
Makoyo,M.S. (2014). ‘‘A Critique of Christian Education for Self Reliance in Kenya i light of Existentialism’’.Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu cha Nairobi.(Haijachapishwa)
Mbithi,J. (1969). .AfricanReligionsandPhilosophy.London:Heinman Education Books Ltd.
Mohamed S.A. (1995). Amezidi. East African Educational publishers. Nairobi.
Nkonge,G.(2006). “ Athari za Udhanaishi katika KichwaMaji na NguvuzaSala” Tasnifu ya Uzamili, Chuo Kikuu cha Nairobi( Haijachapishwa)
Nyamemba,(2012).‘Uchanganuzi Linganishi wa jinsi waandishi katika TunuyaUshairi wanavyoshughulikia masuala ya vijana” Tasnifu ya Uzamili ,Chuo Kikuu cha Nairobi
( Haijachapishwa)
TUKI, (2012). Kamusi ya Kiswahili Sanifu (Toleo la 3)Nairobi. Oxford University.
Walibora,K .(.2012). KidagaaKimemwozea,Nairobi;Target Publication Limited
----------------(2006). KufaKuzikana .Nai robi;Target Publications
Published
2024-05-22